Home Uncategorized MBWANA SAMATTA AKUTANA NA HILI KUTOKA KWA BOSI WAKE MPYA, KAZI ANAYO

MBWANA SAMATTA AKUTANA NA HILI KUTOKA KWA BOSI WAKE MPYA, KAZI ANAYO


DEAN Smith, Kocha Mkuu wa timu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England amesema kuwa mshambuliaji wake Mbwana Samatta ni lazima aongeze juhudi ili kufikia malengo yake.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutoka ardhi ya Bongo kushiriki Ligi Kuu England baada ya kupewa dili la miaka minne na nusu akitokea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

“Samatta anahitaji mazoezi zaidi na kuongeza juhudi kwani hapa alipo ni tofauti na kule alikokuwa, uzuri ni kwamba analitambua hilo na ana kazi ya kufanya,” amesema.

Samatta anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza na timu yake mpya kwenye mchezo wa Jumanne ambao utakuwa ni dhidi ya Leicester ambao ni wa Kombe la Carabao.

Kwenye mchezo huo utakaochezwa Januari, 28, Aston Villa wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Villa Park wanatikiwa kushinda ili kutinga fainali baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  HARMONIZE AWEKA REKODI KUBWA AFRIKA