Home Uncategorized YANGA WAJANJA SANA, WAIPIGA BAO MAZIMA SIMBA KWA KIUNGO WAO MPYA

YANGA WAJANJA SANA, WAIPIGA BAO MAZIMA SIMBA KWA KIUNGO WAO MPYA

BERNARD Morrison, kiungo mpya wa Yanga amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu naye ataongeza mkataba mwingine mrefu ili kuendelea kuwapa burudani.

Inaelezwa kuwa, Morrison alipewa kandarasi ya miezi sita inayotoa nafasi kwa wapinzani watani wa jadi wao Simba kufanya mazungumzo naye endapo watamhitaji.

 Kiungo huyo raia wa Ghana amesema hawezi kuwaangusha mashabiki na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake.

“Nimesaini ndani ya Yana na tayari nimeanza kuzoeana na wachezaji hivyo suala la kusepa kwa sasa halipo na nitazungumza na uongozi ili kujua tunafikia hatua gani hatuwezi kushindwana,”.

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa Yanga umefanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumpa mkataba mrefu utakaomzuia kufanya mazungumzo na timu nyingine.


SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI