Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA AWAVAA WACHEZAJI WAKE TENA, KUMBE LUGHA TATIZO

MBELGIJI WA SIMBA AWAVAA WACHEZAJI WAKE TENA, KUMBE LUGHA TATIZO


SVEN Vanndrbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna tatizo kubwa la mawasiliano kwa wachezaji wake jambo ambalo linawafanya washindwe kupata mabao mengi wakiwa ndani ya Uwanja.

Simba, Jana, Januari 25 iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Mwadui kwenye mchezo wa hatua ya 32 ya Kombe la Shirikisho na kuipa nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Mabao ya Simba yalifungwa na Clatosu Chama na lile la ushindi likifungwa na Francis Kahata huku bao pekee la Mwadui likifungwa na Gerald Mdamu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa walikuwa na nafasi ya kushinda kwa mabao mengi wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata ndani ya kumi na nane.

“Tulikuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi ila wachezaji wangu walishindwa kuwa na mawasiliano mazuri ndani ya uwanja jambo ambalo limewafanya wavune ushindi mwembamba kwenye mchezo wetu ambao tulistahili kufunga mabao mengi zaidi ya haya mawili tuliyopata,” amesema.

SOMA NA HII  KAMA UTANI VILE KOCHA NAMUNGO ABWAGA MANYANGA