Home Uncategorized MANULA AWAPOTEZA MAZIMA MAKIPA WA YANGA

MANULA AWAPOTEZA MAZIMA MAKIPA WA YANGA


AISHI Manula, mlinda mlango namba moja wa Simba, amewapoteza makipa wawili wa Yanga katika kukusanya clean sheet na dakika za kukaa langoni.
Kwenye mechi tatu za hivi karibuni, Manula ametoka na jumla ya clean sheet tatu ndani ya dakika 270, huku Mnata akitumia dakika 180 kwenye mechi mbili na Shikhalo akitumia dakika 90 bila kutoka na clean sheet.
Kuanzia Juni 24, wakati Mbeya City ikikubali kichapo cha mabao 2-0, Juni 28 wakati Tanzania Prisons ikilazimisha sare ya bila kufunganza zote zilichezwa Uwanja wa Sokoine na alimaliza Julai Mosi, wakati Simba inamenyana na Azam FC, Simba ilishinda mabao 2-0 Uwanja wa Taifa na kukusanya clean sheet tatu mfululizo.
Kwa upande wa makipa wa Yanga, Juni 24 wakati Yanga inamenyana na Namungo kwenye sare ya kufungana mabao 2-2, langoni alikaa Mnata,Juni 27 wakati Yanga ikishinda mabao 3-2 mbele ya Ndanda, langoni alikaa Shikhalo na wakati Yanga ikishinda mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar, langoni alikaa Mnata zote zilichezwa Uwanja wa Taifa.

Mechi tatu za Manula zote ameambulia clean sheet huku tatu za Yanga makipa wote wawili wakiruhusu kutunguliwa.

Watakutana Simba na Yanga Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa nusu fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
SOMA NA HII  YANGA YAFANYA MAAMUZI MENGINE KUHUSU AJIBU