Home Uncategorized MTAMBO HUU WA MABAO SIMBA WALETWA SIKU KAMA YA LEO

MTAMBO HUU WA MABAO SIMBA WALETWA SIKU KAMA YA LEO


FRANCIS Kahata, mtambo wa kutengeneza mabao ndani ya Simba leo anasherehekea mfanano wa kuletwa duniani.

Raia huyo wa Kenya alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Gor Mahia amekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu kwa kutimiza majukumu yake.

Pacha yake na rafiki yake wa zamani walipokuwa Gor Mahia na sasa wanaendeleza urafiki ndani ya Simba imetengeneza jumla ya mabao 35 kati ya 69 ambayo yamefungwa na Simba.

Kagere akiwa ni kinara wa utupiaji akiwa  na mabao 19 na pasi tano, Kahata ametupia mabao manne na kutengeneza pasi saba za mabao.

Hizi ni rekodi  za kwenye Ligi Kuu Bara pekee ambapo Simba kwa sasa ni mabingwa wakiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 32 za ligi.

Kwa sasa timu ipo Mtwara ambapo Julai 5 itamenyana na Nndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mchezo wa ligi.

Kwenye mchezo wa kwanza walipocheza na Ndanda Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 2-0 ambapo moja ya bao lilifungwa na mtambo huu wa mabao ulioletwa siku kama ya leo dunia kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 uliomshinda mlinda mlango wa Ndanda FC.

SOMA NA HII  SIMBA YATUMA UJUMBE WA KIBABE KWA NAMUNGO FC