Home Uncategorized MZEE MAGALI ALIVYOMWEKEA UPUPU MWALIMU WAKE

MZEE MAGALI ALIVYOMWEKEA UPUPU MWALIMU WAKE


Mkali wa filamu za Kibongo, Charles Magali ameibuka na kuweka wazi siri aliyokuwa ameificha toka utotoni na kudai kuwa aliwahi kumuwekea mwalimu wake upupu kwenye kiti chake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mzee Magali alisema katika maisha yake alikuwa mbabe tangu utotoni na anakumbuka alipokuwa shule kuna ugomvi ulitokea kati yake na wanafunzi wenzake, mwalimu akampiga kitendo kilichomkera na ndipo akajiapiza kumkomesha mwalimu huyo.

“Nilipotandikwa na mwalimu nilikasirika sana, siku iliyofuata nilisaka upupu na kumuwekea kwenye kiti chake, bila kujua alikikalia akakiona cha moto, kwani alijikuna mpaka akajibandua ngozi, alibaini kuwa ni mimi ndio nilifanya hivyo akahamishia soo nyumbani,” alisema.

Baada ya kesi hiyo kupelekwa nyumbani, baba wa Magali ambaye alikuwa mkali sana aliamua kumuadhibu hali iliyomfanya aamue kuhama nyumba hadi hasira za baba yake zilipoisha ndipo akarudi.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO YANGA KUSHUKA KESHO