Home Uncategorized JIPYA LAIBUKA JUU YA NINJA NA YANGA

JIPYA LAIBUKA JUU YA NINJA NA YANGA


INAELEZWA beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anatakiwa na moja kati ya timu zinazoshiriki
Ligi Kuu ya Zambia lakini amepatwa na kigugumzi kufuatia viongozi wa timu hiyo kumtaka kwanza atulie.

Beki huyo amemaliza mkataba na timu hiyo baada ya kujiunga nayo akitokea Taifa Jang’ombe kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mpaka sasa licha kudaiwa kupata timu nchini Zambia.

Chanzo cha kuaminika kimeliambia Spoti Xtra beki huyo tayari ana ofa za timu za nje ikiwemo Zambia lakini anashindwa kujua cha kufanya baada ya viongozi wa Yanga viongozi kumzuia kuondoka lakini mpaka sasa hajui kama atapewa mkataba.

Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra lilimtafuta Ninja ambaye alisema kuwa: “Niliambiwa nisubirie lakini hadi sasa bado sijapokea simu kutoka kwa viongozi lakini tayari nina ofa kwa timu za nje naweza nikaenda kama nikiona bado wanaendelea kubaki kimya.”

SOMA NA HII  WACHEZAJI BONGO VIWANGO VYAO KUSHUKA IWAPO WATASHINDWA KUFANYA HAYA