Home Habari za michezo YANGA WAMUIBUA KOCHA TABORA UNITED….. JAMBO LAFIKA TFF ISHU NZIMA IKO HIVI

YANGA WAMUIBUA KOCHA TABORA UNITED….. JAMBO LAFIKA TFF ISHU NZIMA IKO HIVI

Kocha Mkuu wa Tabora United, Mserbia Goran Kopunovic amelalamikia kutopewa nafasi ya kuchezea uwanja wa nyumbani licha ya viongozi wa timu hiyo kutengeneza uwanja vizuri.

Goran ameyasema hayo jijini Dodoma jana, Desemba 22, 2023 mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga unaopigwa katika Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 1:00 kesho.

Kocha huyo ameeleza kuwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi upo katika hali nzuri, lakini anashangaa kwanini klabu hiyo haipewi nafasi ya kuutumia jambo lililoifanya kufanya vibaya kwenye baadhi ya michezo ambayo ingekuwa na faida ya kucheza nyumbani.

“Huu ni mchezo wa 13 wa Ligi Kuu na wa 14 pamoja na michezo ya Kombe la Shirikisho, hivyo kati ya michezo yote tumecheza minne pekee nyumbani, huku tukicheza michezo 10 nje ya Tabora kitu ambacho sio sawa kwetu,” ameongeza kocha huyo.

Hata hivyo, tayari Bodi ya Ligi (TPLB) imeshauruhusu uwanja huo kutumika baada ya mchezo wa kesho.

Goran amesema alitegemea kwamba uwanja huo ungeruhusiwa kutumika mapema ili mashabiki wao waishuhudie Yanga mjini Tabora.

“Mimi sipendi kutoa taarifa za uongo, lakini uwanja (wa Ali Hassan Mwinyi) upo kwenye hali nzuri sana na watu wote lazima waelewe kwamba timu hii ni muhimu kwa wana Tabora, lakini sijui kwanini TFF inawanyuma furaha (dhidi ya Yanga),” ameeleza kocha huyo.

Goran ameeleza kuwa wamejipanga vyema kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga akitamba kwamba, wababe hao wa Jangwani wasitegemee kupata mteremko kutoka kwao.

SOMA NA HII  PAPY TSHISHIMBI YUPO TAYARI KUONDOKA YANGA, MKATABA WAKE UMEBAKIZA SIKU 10