Home Simba SC SIMBA KUWAFUATA BIASHARA UNITED LEO

SIMBA KUWAFUATA BIASHARA UNITED LEO

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, leo Februari 16 kitaondoka kwa ndege jijini Dar es Salaam kwenda jijini Mwanza.

 
Kesho Jumatano, Februari 17 kitaelekea mkoani Mara kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kuchezwa Simba  Februari 18, 2021  Uwanja wa Karume.

Gomes amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa ila wanahitaji pointi tatu muhimu.

“Ni mchezo mgumu kwetu hasa ukizingatia kwamba tutakuwa ugenini, haina maana kwamba itakuwa kazi nyepesi hapana.

“Nimewaambia wachezaji kwamba tunahitaji kupata pointi tatu wao wameelewa hivyo tutakwenda kupambana ndani ya uwanja kwa hali na mali,” . 

Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya nne na pointi 32.


SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPIGWA ZENGWE SIMBA ....HIVI NDIVYO BOCCO ANAVYOENDELEA KUTAKATA BONGO...