Home Simba SC GOMES ‘AKUNWA’ NA ‘KOMBINESHENI’ YA MUGALU NA BOCCO

GOMES ‘AKUNWA’ NA ‘KOMBINESHENI’ YA MUGALU NA BOCCO


Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes leo ametumia takribani masaa mawili kukinoa kikosi chake kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Alhamisi kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, huku akitaja kufurahishwa na kombinesheni ya John Bocco na Chris Mugalu.

Katika mazoezi hayo, Mfaransa huyo alielekeza zaidi katika kupiga pasi na kufunga mabao na kusaka pumzi kwa nyota wake, huku Bernard Morison, John Bocco wakiwaacha na shangwe mashabiki waliokuwa wamejitokeza kwenye matizi hayo.

Gomes baada ya mazoezi hayo, amesema kuwa anafahamu mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na wapinzani walivyo, huku akiweka wazi kuwa iwapo watashinda mpambano huo watajiweka katika mazingira ya kutwaa ubingwa huo.

Ameongeza kuwa licha ya mfumo wake kuwa wa 4-3-3, lakini anaridhishwa na kombinesheni ya washambuliaji wake wawili, Bocco na Mugalu na kwamba huenda akaendelea kuwapa nafasi zaidi ila itategemea na mipango yao kulingana na mechi husika.

“Tunahitaji ushindi katika mchezo huo na iwapo tutafanikiwa itatuweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa msimu huu, vijana wangu wako fiti kwa ajili ya mchezo huo, kuhusu Bocco na Mugalu kazi yao ni nzuri” amesema Kocha huyo Mfaansa.

SOMA NA HII  UZEMBE WA MABEKI SIMBA WAMTIA KIWEWE ROBERTINHO....AANZA KAZI NA CHE MALONE...