Home Azam FC KINACHOMBEBA MTUPIAJI NAMBA MOJA BONGO HIKI HAPA

KINACHOMBEBA MTUPIAJI NAMBA MOJA BONGO HIKI HAPA


 NYOTA wa Azam FC, Prince Dube amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ni ushirikiano anaoupata kutoka kwa wenzake kila wakati.

Jana, Juni Mosi, Azam FC walitangaza rasmi kumuongezea dili la miaka miwili nyota huyo, raia wa Zimbabwe hivyo yupo kikosini mpaka 2024.

Ni namba moja kwa utupiaji, akiwa ametupia mabao 14 na pasi tano za mabao, ametengeneza pasi tano za mabao katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Dube pia ana mabao matatu ambayo amefunga kwenye timu yake katika Kombe la Shirikisho na uhakika kwenye hatua ya nusu fainali watakutana na Simba.

Nyota huyo amesema:”Sifanyi haya yote peke yangu ila kikubwa ni ushirikiano ambao ninaupata kutoka kwa wachezaji wenzagu.

“Bado kazi inaendelea na tutazidi kushirikiana zaidi kufikia malengo ambayo tunayo kwani furaha yetu ni kuona tunapata matokeo chanya,” amesema Dube.

SOMA NA HII  LWANDAMINA AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA SIMBA