Home news HIZI HAPA SABABU ZA MAYELE KUAMUA KURUDI KWAO CONGO…ADAI HACHEZI PEKE YAKE….

HIZI HAPA SABABU ZA MAYELE KUAMUA KURUDI KWAO CONGO…ADAI HACHEZI PEKE YAKE….


STRAIKA nyota wa Yanga, Fiston Mayele anatarajia kuukosa mchezo wa kwanza wa Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe kutokana na kuondoka kikosini humo na anatarajia kuungana tena na timu Januari 7 mwaka huu.

Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji juzi Ijumaa, Mayele alipanga kuondoka kwenda Congo kuhani msiba wa shemeji yake na amesema kuwa ataungana na timu visiwani Zanzibar baadaye.

Yanga inatarajia kutupa karata yake ya kwanza kwenye mashindano hayo dhidi ya Taifa Jong’ombe Januari 5 katika mechi itakayopigwa Saa2:15 usiku ndani ya Uwanja wa Amaan, mjini Unguja.

Mayele alisema kukosekana kwake kwenye mchezo huo haiondoi Yanga kuibuka na ushindi kutokana na timu hiyo kusheheni wachezaji wenye uchu wa matokeo mazuri kwenye kila mchezo. Yanga ndio watetezi wa michuano hiyo ikipangwa Kundi B ikiwa pia na KMKM.

“Sichezi peke yangu kwenye timu tunacheza wengi na timu imesajili kikosi kipana ikizingatia wingi wa mashindano hivyo natarajia kusikia matokeo mazuri ya kunifariji nikiwa Congo,” alisema Mayele na kuongeza;

“Yanga mipango yetu ni kutwaa kila taji lililo mbele yetu hivyo tunatarajia mambo makubwa kwenye kila mashindano ikiwa ni sambamba na ushindani hilo halitatukatisha tamaa tutapambana mwanzo hadi mwisho lengo ni kuona mashabiki zetu hawakauki furaha hii ni kutokana na namna wanavyotuamini.”

SOMA NA HII  YANGA KUTUMA UJUMBE AFRIKA NZIMA JUMAPILI HII, ALLY KAMWE ATAMBA