Home news USAJILI WA NKANE YANGA WAZUA JAMBO…UONGOZI WAGUSIA KUTEMA MCHEZAJI…

USAJILI WA NKANE YANGA WAZUA JAMBO…UONGOZI WAGUSIA KUTEMA MCHEZAJI…


Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema hana budi kumtoa kwa mkopo kiungo mmoja katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Nabi ameweka wazi mpango huo kabla ya kuondoka nchini kuelekea Ubelgiji kujiunga na familia yake kwa mapumziko katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu imesimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Kocha huyo kutoka Tunisia amesema usajili wa kiungo Dennis Nkane aliyetokea Biashara United Mara unamsukuma kufanya maamuzi hayo ya kumpunguza mchezaji mmoja.

“Kwa sasa tutakuwa na jumla ya mawinga watano, naangalia uwezekano wa kumtoa mmoja ili timu iwe na uwiano mzuri tubaki na wanne.”

Mbali na Nkane, mawinga wengine ni Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko na Deus Kaseke

SOMA NA HII  WAKATI ONANA AKIPIGWA BEI ....KITASA CHA ASEC MIMOSAS KUMRITHI INONGA SIMBA...