Home Habari za michezo SHAFFIH DAUDA:- SIMBA WANGEANZA NA KIBU DENIS…WAARABU WANGEKOMA…

SHAFFIH DAUDA:- SIMBA WANGEANZA NA KIBU DENIS…WAARABU WANGEKOMA…

Habari za Simba

Wakati kila Shabiki wa klabu ya Simba akiwa hana matumaini na ubora wa mchezaji kama Kibu Denis hali ni tofauti kwa mchambuzi nguli wa Sika nchini Shaffih Dauda.

Akizungumza Shaffih katika kipindi cha hili game kinachhorushwa na Redio Clouds wakati wakieleza sababu hasa za Simba kupoteza mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Raja Casblanca jumamosi iliyopita amesema;

“Hakuna kazi ngumu kana kumsoma mpinzani na kutengeneza Timu ya kucheza , kwa Simba juzi huwezi ukahukumu kwa kupoteza mechi, Mimi ukiniuliza nafikiri kosa la kwanza ni selection ya Timu ( Upangaji wa Kikosi) ilikuwa ni kosa la Jinai kwangu kumuweka kwa wakati mmoja Bocco , Saido, Chama na Sakho katika eneo la mbele “

“Mpira wa kisasa takwimu zinasema mchezaji anayefanya kazi muda wote ni huyu wa mbele , katika dakika 90′ atakimbia dakika 60′, Saido ili awe bora anamuhitaji Kibu , kwangu Mimi mchezaji wa kwanza kwenye kikosi angekuwa Kibu, Kibu ni mchezaji ambaye wengi hawampendi lakini anafaida kubwa”-

SOMA NA HII  KIGOGO SIMBA AMTABIRIA MAKUBWA INONGA

1 COMMENT