Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA KUILIPA SIMBA KWA MAGOLI….MOSES PHIRI AIBUKA NA HILI TENA…AOMBA...

BAADA YA KUANZA KUILIPA SIMBA KWA MAGOLI….MOSES PHIRI AIBUKA NA HILI TENA…AOMBA UTAMBULISHO MPYA…


Mzambia Moses Phiri anayekipiga Simba yupo moto, kwani jamaa anatupa tu mipira nyavuni kila akishuka uwanjani na mwenyewe ametamba ‘na bado, nitafunga sana, kwani ndio kazi yangu’.

Phiri aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Zanaco, amefunga mabao manne katika mechi nne za kimashindano, zikiwamo tatu za Ligi Kuu Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mwenyewe ameweka wazi kuwa hicho ndicho kilichomleta Msimbazi na ataendelea kutupia sana tu.

Mshambuliaji huyo juzi aliifungia Simba bao la kwanza katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets akibinuka tikitaka kabla ya nahodha John Bocco kutokea benchi na kufunga bao la pili lililowapa Wekundu hao ushindi wa mabao 2-0 ikiwa ugenini.

Akizungumza Phiri alisema mabao ndio kitu kilichomleta Simba na yupo hapo ili kufunga zaidi na kuifanya timu ifikie malengo.

“Hata huko nilikokuwa (Zanaco) nilifunga ndio maana Simba ikaniona na kunisajili kwa sababu hiyo hivyo nahitaji kufunga zaidi na kuifanya timu ifikie malengo kwani ndicho kitu kilinileta hapa,” alisema Phiri anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu hadi sasa akiwa na matatu sambamba na Reliants Lusajo wa Namungo na Matteo Anthony wa KMC.

Nyota huyo pia amewatoa hofu mashabiki na wadau wanaohoji eneo lake rasmi la kucheza uwanjani wengi wakisema sio mshambuliaji wa mwisho bali ni namba 10 lakini yeye amelitolea ufafanuzi hapa.

“Mpira ni kazi yangu hivyo siwezi kuchagua eneo la kucheza, nakumbuka nimewahi kucheza kama namba mbili, nikacheza kama kiungo namba sita tena Ulaya baadae winga, namba 10 na sasa Mshambuliaji.

Najivunia kuwa na uwezo wa kucheza maeneo yote lakini kwa sasa nacheza zaidi eneo la ushambuliaji hivyo naomba wanitambue kama Mshambuliaji wa Simba,” alifafanua Phiri na kuongeza;

“Nafurahia kucheza eneo hili, lakini kikubwa zaidi nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano wao kama timu na mashabiki wasiwe na hofu tena juu ya hilo.”

Phiri ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Simba msimu huu akitokea Zanaco ya kwao Zambia alikomaliza ligi na mabao 14 na msimu mmoja nyuma aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu Zambia akicheka na nyavu mara 16.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA 'KUSHAINI' SIMBA...MORRISON ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU PABLO...AMSHUSHIA...

Ubora wa Phiri kwa sasa unazidi kuiimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba inayounda na yeye, Dejan Georgijevic, Habib Kyombo na Bocco.