Home Yanga SC KISA USAJILI MPYA WA YANGA..ZAWADI MAUYA AFUNGUKA HAYA..AMTAJA NIYONZIMA

KISA USAJILI MPYA WA YANGA..ZAWADI MAUYA AFUNGUKA HAYA..AMTAJA NIYONZIMA


KIUNGO mkabaji wa Yanga, Zawadi Mauya amesema amefurahishwa na majembe yanayoshuka Jangwani yanaashiria msimu unaokuja (2021/22), timu yao itanyakua mataji ya mashindano mbalimbali.

Mauya amesema kwamba mabosi wake wameshusha majembe ya maana yatakayounganisha nguvu na wachezaji waliokuwepo msimu ulioisha.

“Viongozi wetu wamefanya usajili mzuri, wamekuja kutupa nguvu ya kuanza ligi ijayo kwa kishindo cha kunyakua mataji ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam na mengineyo,” amesema Mauya na ameongeza kuwa;

“Najua utakuwa ni msimu mgumu ambao tutakuwa mwiba kwa wapinzani wetu, kwani tuna hamu, ujue kuna msemo wa wahenga mwenye shibe hamjui mwenye njaa, sisi tuna njaa ya mataji,” amesema.

Msimu wa 2021/22 utakuwa msimu wa pili wa Mauya ambaye aliwapa raha Wanayanga baada ya kuitandika Simba bao 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, mechi ya mzunguko wa pili.

Lakini pia aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima ni kama alimtabilia makubwa Mauya kwa kutaka avae jezi yake (No 8), akiona itafiti kutokana na kile anachokiona mguuni kwake.

Alipoulizwa amejipangaje kulifanyia kazi hilo msimu ujao!! Alijibu kuwa “Niyonzima alikuwa na majukumu mazito, kipaji chake kilikuwa kikubwa, atapambana na anamuahidi hatamuangusha,” amesema.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO WA YANGA KUTUA LEO