Home Habari za michezo KUHUSU KUSEPA YANGA…MAYELE AVUNJA UKIMYA….AANIKA ATAKAPOKUWA MSIMU UJAO…

KUHUSU KUSEPA YANGA…MAYELE AVUNJA UKIMYA….AANIKA ATAKAPOKUWA MSIMU UJAO…

Habari za Yanga

Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fisto Mayele amepata kigugumizi na kushindwa kujibu iwapo ataendelea kusalia Yanga msimu ujao ama ataondoka kutokana na kiwango chake kuwa bora zaidi msimu huu.

Mayele amesema hayo jijini Dar wakati akihojiwa na wanahabari mara baada ya kuwasili nchini na kikosi hicho wakitokea Algeria ambako walikuwa wakicheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) ambapo USM Alger waliibuka mabingwa wa michuano hiyo juzi Jumamosi, Juni 3, 2023.

Aidha, Mayele amekuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa na mabao saba huku pia akiongoza katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 16 wakati anayefuata ana mabao 10.

“Ni furaha sana kwangu na binafsi ninajipongeza, ukiwa unafanya kazi na ukawa na malengo ya kufika stage flani na ukafanikiwa basi ni jambo kubwa la kumshukuru Mungu.

“Mchezaji anakuwa kwenye performance nzuri kwa miaka miwili mfululizo sio rahisi, kuna mahitaji mengi sana lazima kuna vitu vya kufanya na si vya kufanya ili ufanye vizuri.

“Bado kuna mechi mbili za Ligi na nikichukua tena kiatu cha ufungaji bora Ligi ya Tanzania utakuwa ni msimu wangu bora sana tangu nianze ucheza mpira.

“Kuhusu kuendelea kuwa Yanga msimu ujao au kuondoka nadhani sasa hivi sio wakati wake kuzungumzia kwa sababu bado hatujamaliza msimu tuna mechi mbili za Ligi na fainali ya FA, baada ya hapo tunaweza kukaa mezani kuangelea hilo jambo,” amesema Mayele.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI