Home Uncategorized BREAKING:KIWIKO CHAMPELEKA MORRISON KAMATI YA NIDHAMU

BREAKING:KIWIKO CHAMPELEKA MORRISON KAMATI YA NIDHAMU


KIUNGO Mshambuliaji Bernard Morrison anayekipiga ndani ya Yanga  amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons FC Jeremia Juma.

Morrison alifanya hivyo wakati mpira ukiwa umesimama kwenye mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikamilika kwa Yanga kugawana pointi moja na Prisons baada ya kuisha kwa sare ya bila kufungana.

SOMA NA HII  Baada ya Bocco, Simba kutangaza mwingine leo!