Home kimataifa ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI

ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atlanta kwenye mchezo wao uliochezwa Februari 24 ni utimamu wa mwili wa wachezaji wake pamoja na matumizi ya nguvu.


Zidane amesema:-“Wachezaji walikuwa timamu sana kimwili na matumizi makubwa ya nguvu jambo ambalo limeweza kuwapa ushindi ndani ya uwanja.

 “Pia jambo jingine ilikuwa ni kuweza kuongeza nguvu kwa upande wa kujilinda hilo nalo ni muhimu kwao hivyo wanastahili pongezi,”.


Ni mchezaji wao Remo Freuler dakika ya 17 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Atlanta kumaliza wakiwa pungufu kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Atletti Azzurri d’italia.

 Kwa upande wa kocha wa Atalanta, Giann Piero Gasperini ameoneshwa kutokufurahishwa na matokeo hayo kwani yalikuwa nje ya matarajio yao. 


“Nimesikitishwa kwa kutoweza kuucheza mchezo kama tulivyotaka. Ulikuwa mchezo tofauti baada ya kuwa pungufu. Tukapaswa kujilinda zaidi.

 

 “Tunapaswa kushinda kwenye mchezo wa marudiano Madrid, ni rahisi hatupaswi kufikiria sana. Tuna uwezekano mmoja tu, tunapaswa kushinda”.

 

Atalanta ina kazi nyingine tena Machi 16 mwaka huu wakati watakapokutana tena na Real Madrid nchini Hispania kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua hiyo ya 16 bora ya michuano hiyo.

 Ni beki wa kushoto wa Real Madrid, Ferland Mendy alipachika bao la ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya.

 Mendy alifunga bao hilo dakika nne kabla mchezo kumalizika baada ya kupokea pasi ya Luka Modric akiwa nje ya eneo la 18 na kupiga mpira kwa ustadi mkubwa uliomshinda mlinda mlango wa Atalanta, Pierluigi Golini na kutinga wavuni.

 

Bao hilo ni kwanza kwa Mendy aliyecheza michezo 20 kwenye michuano hiyo pekee, ilhali ni la pili kwenye michezo 22 aliyecheza kwenye michuano yote msimu huu akiwa na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania.

SOMA NA HII  PEP GUARDIOLA KUSEPA MANCHESTER CITY

 


Kwa upande wa rekodi, Real Madrid imepata ushindi wake wa kwanza kwa Atalanta, kwani wawili hao walikuwa wanakutana kwa mara yao ya kwanza huku Atalanta ikiweka rekodi ya kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango