Home news RAIS KARIA KUTOA DONGE NONO

RAIS KARIA KUTOA DONGE NONO


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walles Karia ametangaza kutoa donge nono la sh.milioni kumi kwa Mwenyekiti bora wa chama cha wa mpira ngazi ya mkoa atakayefanya vizuri kuliko wengine baada ya kukidhi vigezo vitakavyowekwa kuwashindanishwa.

 Mpango mkakati huo ni moja wapo ya  malengo aliyoyatangaza Rais Karia mara baada ya kutawadhwa kuongoza tena Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne mingine katika uchaguzi mkuu uliofanyika juzi Jumamosi mkoani Tanga akipitishwa kwa asilimia 100.

Karia alisema kwa miaka minne aliyoongoza Shirikisho hilo kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwajibika ipasavyo kwa viongozi wanaoongoza vyama vya mpira wa miguu mikoani ambapo alisema awamu hii hawataki kurudi nyuma tena watahakikisha wanaimarisha utendaji.

“Ninatangaza kutoa shilingi milioni kumi kwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa atakayefanya vizuri zaidi kushinda wengine, tutakwenda kuandaa vigezo ambavyo tutavitumia kumpata mshindi lengo la kufanya ushindani huu ni kuongeza ufanisi kwa watendaji ili kuweza kuinua mchezo huu,” alisema Karia.

Aliongeza kuwa: “Sisi shirikisho tuna  mahusiano mazuri na wizara yenye dhamana ya michezo lakini huko mikoani na wilayani hakuna mahusiano mazuri kati ya vyama vya siasa na  viongozi wa Serikali, niwaombe kujenga ukaribu zaidi ili tuwe katika mstari mmoja kuliendeleza soka letu la Tanzania,” alisema Karia. 

Mara Baada ya kutangazwa kuwa Rais,  Karia ametangaza Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri hiyo mmoja wapo ni Mwanamama Hawa Mniga ambaye pia alitia nia ya   kugombea katika nafasi ya Urais wa Shirikisho.

SOMA NA HII  ABDALLAH ASHINDA JACKPOT YA SPORTPESA