Home kimataifa AUBA ANA TUZO KIBAO KABATINI,BUNDESLIGA ALICHEZA MECHI 144

AUBA ANA TUZO KIBAO KABATINI,BUNDESLIGA ALICHEZA MECHI 144


 NYOTA wa timu ya taifa ya Gabon ambaye ni mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Aubameyang rekodi zinaonyesha kwamba alicheza mechi nyingi ndani ya Klabu ya Borussia Dortmund ambazo ni 144.


Dortmund ambayo inashiriki Bundesliga iliweza kushuhudia jumla ya mabao 98 ambayo aliyafunga na pia alitoa jumla ya pasi za mabao 22 katika mechi hizo 144.

Ubora wake ndani ya Bundesliga uliwafanya mabaosi wa Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England kumvutia waya na kuinasa saini yake ilikuwa msimu wa 2018.

Mpaka msimu uliopita wa 2020/21 nyota huyo ndani ya Arsenal alicheza jumla ya mechi 114 na alitupia jumla ya mabao 64.

Mkataba wake ndani ya Arsenal unatarajiwa kumeguka rasmi Juni 30,2023.Ana tuzo moja ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka, ametwaa taji moja la FA, ana tuzo mbili za ufungaji bora msimu wa 2018/19 alitupia mabao 22 ndani ya Ligi Kuu England na 2016/17 alitupia mabao 31 ndani ya Bundesliga.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA ARSENAL, LACAZETTE AINGIA ANGA ZA BARCELONA