Home epl MSHAMBULIAJI WA ARSENAL, LACAZETTE AINGIA ANGA ZA BARCELONA

MSHAMBULIAJI WA ARSENAL, LACAZETTE AINGIA ANGA ZA BARCELONA

IMERIPOTIWA kwamba nyota wa Klabu ya Arsenal, Alexandre Lacazette anawaniwa na timu nyingi nje ya klabu hiyo ikiwa ni pamoja na Barcelona, Juventus na Atletico Madrid.

Kwa sasa Lacazette mkataba wake ndani ya kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Mikel Arteta unakaribia kufika ukingoni msimu huu wa 2020/21 na amekuwa hana uhakika wa namba kikosi cha kwanza kwa kuwa wakati mwingine amekuwa akianza na mwingine amekuwa akianzia benchi.

Mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao nane ndani ya Ligi Kuu England. Habari zinaeleza kuwa nyota huyo yupo tayari kuondoka katika Ligi Kuu England ili kupata changamoto nyingine nje ya Emirates.

Hivyo upo uwezekano nyota huyo akaibukia ndani ya Serie A kwa wababe Juventus ikiwa atakubali kusaini huko ama ndani ya La Liga kwa Barcelona ama Atletico Madrid ambazo zote zimeonyesha nia ya kuipata saini yake.

Kwa mujibu wa Calciomercato.Com umeeleza kuwa Lacazette yupo tayari kuondoka ndani ya Arsenal mkataba wake utakapoisha.


SOMA NA HII  LUKAKU AKWEA PIPA KUIBUKIA LONDON