Home Uncategorized SAKATA LA MORRISON LAIBUKA UPYA KABISA

SAKATA LA MORRISON LAIBUKA UPYA KABISA

 


UONGOZI wa Yanga, umerudi tena Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiandika barua kuomba majibu ya ukiukwaji wa usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Morrison kwenye mfumo wa TMS.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kiungo wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya aliyesajiliwa na timu hiyo usajili wake kuonekana na matatizo kabla ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) sambamba na kutozwa faini ya dola 130,000 (Sh 300Mil).


Kichuya alijiunga na Simba, Januari, mwaka huu akitokea Pharco ya Misri huku taarifa zikisema aliondoka bila ruhusa. Kwa sasa anaitumikia Namungo FC.

 

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Yanga ambayo Spoti Xtra imeiona, imeandikwa Desemba 4, mwaka huu kwenda TFF kuomba majibu ya barua yao waliyoiandika Septemba 28, 2020 juu ya ukiukwaji wa usajili wa Morrison.

 

Barua hiyo imeandikwa baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kuamuru Morrison kuwa huru baada ya kubainika mkataba wake na Yanga kuonekana una upungufu.


Baada ya mkataba huo kuonekana na upungufu, kamati hiyo ilimruhusu Morrison kujiunga na Simba msimu huu, akisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, ilieleza Yanga imejiridhisha bila shaka Morrison alisajiliwa na Simba kwa makosa yaleyale au zaidi, hivyo kuiomba kamati kufanya maamuzi kama waliyoyafanya kwa Yanga.

 

Aidha, barua hiyo ilieleza kuwa Yanga wanataka kupata ufafanuzi na maamuzi yafanyike kwa Klabu ya Simba kama yalivyofanyika kwao, hiyo ni baada ya kupita muda mrefu bila ya kutolewa majibu hivyo, klabu hiyo inaomba kupatiwa taarifa ya maendeleo ya suala hilo na majibu stahiki kabla ya usajili wa dirisha dogo kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

 

Yanga imeonekana kushtukia jina la kiungo huyo kuingizwa kwenye mfumo wa TMS katika dirisha dogo la usajili baada ya kupata taarifa za jina la Mghana huyo kutokuwepo katika mfumo baada ya usajili mkubwa kushindikana kuliingiza jina lake.

SOMA NA HII  BALAA LA NAMUNGO NA YANGA LEO ACHA KABISA MAJALIWA

 

Endapo itabainika kuna mapungufu hayo, huenda Morrison naye akafungiwa kama ilivyo kwa Kichuya aliyefungiwa kutocheza soka kwa kipindi cha miezi sita.