Home Uncategorized MARCUS RASHFORD AFURAHIA MAISHA YA MANCHESTER UNITED

MARCUS RASHFORD AFURAHIA MAISHA YA MANCHESTER UNITED


NYOTA wa Klabu ya Manchester United, Marcus Rashford amesema kuwa anahitaji kumaliza maisha yake ya mpira wa ushindani akiwa ndani ya timu hiyo kwa kuwa anaipenda.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Manchester City pamoja na Chelsea ambao walikuwa wanatajwa kuwa wanahitaji saini yake.

Rashford amekuwa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupandishwa kutoka kwenye Academi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England ambapo kesho itakuwa na mchezo dhidi ya Manchester Cty Uwanja wa Old Trafford.

Ikiwa ipo nafasi ya sita na pointi zake 19 inakutana na City iliyo nafasi ya 7 na pointi zake 18 jambo linalomaanisha kwamba mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.


Rashford amesema:”Sijawahi kufikiria kuwa nje ya Old Trafford kwa kuwa nilikuwa ninafurahia maisha ya hapa tangu zama zile nikiwa mtoto, ninapenda maisha ya hapa nilipo.

“Kwenye akili zangu sijawahi kufikiria kuhusu siku moja kutoa uzi ambao ninao kwa sasa na kuvaa uzi mwingine, sijafikiria timu nyingine ya kwenda zaidi ya Manchester United.

“Nina matumaini ya kufanya vizuri zaidi hapa nilipo kwa sasa na hilo linawezekana kwa kuwa uwezo na nia ipo,” .

SOMA NA HII  YANGA WATAJA MADENI YAO MAKUBWA MATATU