Home Uncategorized NGORONGORO HEROES LEO KUANZA KAZI NA SAUDI ARABIA

NGORONGORO HEROES LEO KUANZA KAZI NA SAUDI ARABIA

 


KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes tayari kimeanza mazoezi chini ya Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelo wengi wanapenda kumuita Julio na leo kitamenyana na timu ya Saudi Arabia. 


Ngorongoro Heroes imeanza mazoezi katika Mji wa Al Khoba uliopo Mashariki mwa Saudi Arabia ilipowekwa kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Afcon.


Timu hiyo ilikaa siku mbili bila kwa kufanya mazoezi ya ndani ikifanya mazoezi ya Gym kwa kuwa ilikuwa chini ya uangalizi kutoka Serikali ya Saudi Arabia juu ya Covid 19 na wamechukuliwa vipimo na kuonekana wapo salama.


Tayari kwa sasa timu imeanza mazoezi Kwenye Uwanja wa kawaida baada ya kumaliza taratibu za kuwa chini ya uangalizi. 


Ngorongoro Heroes inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki leo na wenyeji wao Saudi Arabia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo ya vijana na haitakuwa na mashabiki.

SOMA NA HII  TFF YATOA ONYO KWA YANGA