Home Taifa Stars PAMOJA NA KUKURUKAKARA ZOOTE ZILE…STARS YAZIDI KUDIDIMIZWA FIFA….GUU LA MANE LAIPAISHA SENEGAL…

PAMOJA NA KUKURUKAKARA ZOOTE ZILE…STARS YAZIDI KUDIDIMIZWA FIFA….GUU LA MANE LAIPAISHA SENEGAL…


Tanzania imeporomoka kwa nafasi moja katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA) kwa mwezi Januari.

Kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka vya Januari vilivyowekwa hadharani jana, Tanzania imeanguka kutoka nafasi ya 131 iliyokuwepo mwishoni mwa mwaka jana hadi nafasi ya 132 ikipishana na Comoro ambayo awali ilikuwa katika nafasi hiyo.

Kufanya vizuri kwa Comoro katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika huko Cameroon mwaka huu, kuimeirudisha nchi hiyo katika nafasi ya 131 na kuichomoa Tanzania ambayo haikushiriki.

Gambia ambao walionyesha kiwango bora na kuishia katika hatua ya robo fainali kwenye fainali za Afcon mwaka huu, juhudi zao zimewalipa kwani imejikuta ikipanda kwa nafasi nyingi na kuwatoa shimoni walipokuwepo awali.

Kutoka nafasi ya 150 waliyokuwepo awali, Gambia wamepanda hadi nafasi ya 125 ikimaanisha wamepaa kwa nafasi 25 zaidi.

Usemi wa chanda chema huvikwa pete, unaweza kutumika pia kwa mabingwa wapya wa Afcon, Senegal ambao wamepaa kwa nafasi mbili kutoka ile ya 20 hadi nafasi ya 18 kidunia huku wakiongoza kwa upande wa Afrika.

Hakuna mabadiliko katika nafasi tatu juu kidunia ambapo Ubelgiji wameendelea kutamba, wakifuatiwa na Brazil katika nafasi ya pili huku wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa ni Ufaransa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA UGANDA...KOCHA TAIFA STARS ATAMBA KUANDAA 'PILIPILI KICHAA' NYINGI ZA USHINDI....