Home news KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…MO DEWJI AKUNJUA POCHI SIMBA….ATOA AHADI YA MAMILIONI..BOCCO AJIFUNGA...

KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…MO DEWJI AKUNJUA POCHI SIMBA….ATOA AHADI YA MAMILIONI..BOCCO AJIFUNGA ULIMI..


KATIKA kuhakikisha wanapata ushindi wa kwanza nyumbani dhidi ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Rais wa Heshima wa Simba, bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’, ameahidi kuwapa bonasi nzuri inayofikia Sh 200Mil kama wakifanikiwa kuwafunga wapinzani wao hao.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili hii saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba ambao ni wenyeji katika mchezo huo, watawakosa wachezaji wake muhimu wenye majeraha Chris Mugalu, Kibu Denis na Clatous Chama ambaye kanuni zinambana kucheza michuano hii kutokana na kucheza mechi za michuano ya Caf akiwa na RS Berkane ya Morocco.

Bosi huyo juzi alivamia kambi ya timu hiyo iliyopo Bunju, nje kidogo ya Dar es Salaam, saa chache kabla ya kuelekea mazoezini kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji hao.

Mara baada ya kuvamia kambini hapo alifanya kikao na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’,

Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na mjumbe wa bodi, Mramu Ng’ambi. Chanzo chetu kimetudokeza kuwa katika kikao hicho, Mo alitoa ahadi hiyo ya bonasi kama wakifanikiwa kupata ushindi wa nyumbani dhidi ya Asec.

“Morali ya wachezaji itaongezeka katika kuelekea mchezo wetu dhidi ya Asec ni baada ya maneno mazuri waliyoambiwa wachezaji wetu na Mo ambaye ni mwekezaji wetu.

“Wachezaji wote walihimizwa kupambana katika mchezo huu ili kuhakikisha tunafuzu katika hatua hii na kufuzu kufika nusu fainali, wachezaji chini ya nahodha Bocco (John) walitoa ahadi nzito kwa Mo na kuahidi kupambana kupata ushindi.

“Ahadi hiyo ya Mo imeongeza morali kwa kila mchezaji aliyepo kambini,” kilisema chanzo hicho.

MO AFUNGA KUELEKEA MCHEZO HUO

“Mimi nimetoka mbali na hii Simba, nashangaa hao watu wanaosema kuwa mimi nimeondoka Simba, nilianza kuipenda timu hii tangu nikiwa mdogo.

“Nimewekeza pesa nyingi ndani ya Simba nilianza kwa kuweka Sh 25Bil lakini kabla nilikuwa nilishatumia 20Bil kabla ya kuongezea Sh 20Bil, hivyo hadi hivi sasa nimefikisha 85Bil ambazo nimetumia katika kipindi changu nikiwa na timu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA TRY AGAIN KUINGILIA KATI...ONYANGO NA SIMBA BADO MAMBO MAGUMU AISEE....ATAKA KUVUNJA MKATABA...

“Lipo wazi kuiendesha klabu kubwa kama ya Simba ni hasara, lakini naendelea kutoa pesa zangu kwa ajili ya Simba, hivyo mimi nipo Simba.

“Tuliteleza kidogo katika msimu huu na kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia huku Shirikisho, malengo yetu ni kufika mbali zaidi ya hapa tulipofikia.

“Tunafahamu tuna majukumu mengi, ikiwemo ligi lakini ninaamini tutapambana, ni lazima  tujipange kwani haya mashindano ni magumu na siriazi.

“Bado tunaendelea kupambana na bajeti yetu ya Simba ili timu iweze kujiendesha yenyewe na kwa miaka minne niliyokuwa kiongozi ndani ya Simba ambayo hivi sasa sina mamlaka nayo sana baada ya kujiondoa katika nafasi ya mwenyekiti wa wakurugenzi, lakini bado nipo ndani ya timu kwa ajili ya kuwasaidia, hivyo niwaambie kuwa nitaendelea kuisadia timu yangu ya Simba.

“Lengo ni kuweka bajeti kubwa ndani ya timu hiyo ili tuweze kupambana na baadhi ya klabu kubwa katika Ukanda wa Afrika kama vile Al Ahly.

“Wengi wanasema mafanikio ya Simba ni Mo lakini mimi naamini mafanikio ya Simba ni mashabiki. Wajitokeze kwa wingi Jumapili. Kiingilio cha chini ni Sh 5,000 lakini natangaza kushusha hadi Sh 3,000,” alisema Mo.