Home Yanga SC YANGA: LIGI ILIANZA VIZURI, ILA MWISHONI IMEPOTEZA MVUTO

YANGA: LIGI ILIANZA VIZURI, ILA MWISHONI IMEPOTEZA MVUTO


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa msimu wa 2020/21 Ligi Kuu Bara ilianza vizuri ila ilipoteza mvuto mwishoni.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 na kinara ni Simba mwenye pointi 64 baada ya kucheza mechi 26.

Ikumbukwe kwamba moja ya mchezo ambao uliyeyuka ni ule uliopaswa kuwakutanisha Simba v Yanga ambapo kutokana na kubadilishwa muda ghafla, Yanga waligomea kucheza mchezo huo kwa kueleza kuwa kanuni hazijazingatiwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa baada ya ratiba kupangwa upya na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB).

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema:”Ligi imepoteza mvuto hapa mwishoni kutokana na ratiba kutokuwa rafiki, yaani haijengi ile fairness katika mpira.

“Tusingeibua ile ishu kuwa kuna timu ambazo hazijacheza mechi zao sijui ingekuwaje.Kama ratiba ingekuwa nzuri zaidi tunaamini kwamba ligi ingekuwa nzuri kama ratiba itakuwa nzuri zaidi ligi itakuwa bora zaidi,” .

SOMA NA HII  SAKATA LA KISINDA...YANGA WAZIDI KUKOLEZA MOTO...WAENDELEA KUTUPA MADONGO TFF KWA NAMNA WALIVYOWAGEUKA...