Home news BAADA YA KUIONA SIMBA IKIPATA USHINDI WA TAABU JANA…’TRY AGAIN’ ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA...

BAADA YA KUIONA SIMBA IKIPATA USHINDI WA TAABU JANA…’TRY AGAIN’ ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA TAMKO JIPYA..


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ ametoa pongezi kwa wachezaji wa klabu hiyo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, uliopatikana jana Jumatano (Novemba 03).

Simba SC ililazimika kusubiri hadi dakika ya 90 ya mchezo huo, uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kupata bao hilo la ushindi kupitia kwa Mshambuliaji wao kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere.

Try Again’ ametoa pongezi kwa wachezaji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, huku akisisitiza bado kuna kitu hakipo sawa kikosini.

Kiongozi huyo ameandika: “Alhamdulilah Lakini Bado Kuna Kitu Hakipo Sawa!!”

“Well done team and good job @mediekagere_officialaccount”

‘Try Again’ hakuishia hapo akaandika tena: “Alama tatu safi zimepatikana #NguvuMoja @mediekagere_officialaccount”

Ushindi huo umeiwezesha Simba kufikisha alama 11 na kukwea hadi nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Young Africans wakiwa kileleni kwa kufikisha alama 15.

SOMA NA HII  AL HILAL YAIBAMIZA MABAO 2-1 TP MAZEMBE, SIMBA SUPER CUP