Home kimataifa CHRISTIAN ERIKSEN ATUMA UJUMBE KWA WACHEZAJI

CHRISTIAN ERIKSEN ATUMA UJUMBE KWA WACHEZAJI


CHRISTIAN Eriksen amewaambia wachezaji wenzake wa Klabu ya Inter Milan kwamba yupo vizuri baada ya kuanguka uwanjani katika mchezo wa Euro 2020 wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Denmark dhidi ya Finland.

Nyota huyo mwenye miaka 29 alianguka uwanjani dakika ya 43 na alipewa huduma ya kwanza na kupelekwa hospitali ambapo wachezaji wenzake waliweza kupata mshtuko na wengine kulia huku wakiunda duara ili kuzuia tukio hilo lisiweze kuonekana.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Parken, ulisoma Denmark 0-1 Finland na mtupiaji alikuwa ni Joel Pohjanpalo aliyepachika bao hilo dakika ya 59. Baada ya tukio hilo alichukuliwa na kupelekwa hospitali kwa huduma zaidi.

Baada ya kuamka amewatumia ujumbe wachezaji wenzake wa Inter Milan pamoja na wale wa timu ya taifa ya Denmark kwamba yupo katika hali nzuri hivyo wasiwe na mashaka juu yake.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Italia, Tancedi Palmeri amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba Eriksen ametuma ujumbe kwenye kikosi cha timu ya Inter Milan kwa kuwaambia kwamba, ‘nipo vizuri’.


SOMA NA HII  CHELSEA YACHEKA UNITED MAJANGA