Home Yanga SC YANGA HAWAJAKATIA TAMAA UBINGWA WA SIMBA

YANGA HAWAJAKATIA TAMAA UBINGWA WA SIMBA


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba bado una matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Simba licha ya kwamba wapo nafasi ya pili.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ni mabingwa watetezi kwenye msimamo wapo nafasi ya kwanza na pointi zao ni 67 baada ya kucheza mechi 27.


Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ipo nafasi ya pili na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29.

 Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado hawajakata tamaa suala la ubingwa wataendelea kupambana.

“Tupo kwenye ligi na bado haijaisha jambo ambalo linatufanya tuamini kwamba bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa kwani kila kitu kinawezekana.
“Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi pia tutapambana kwa mechi zetu na kupata ushindi mwisho wa siku tutajua kile ambacho tumekipata,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA AKILI YOTE KWA SIMBA, LIGI KUU SASA NI VISASI TUPU