Home Azam FC DILI LA KAHATA KUIBUKIA AZAM FC LIMEKUWA GUMU

DILI LA KAHATA KUIBUKIA AZAM FC LIMEKUWA GUMU


 MABOSI wa Azam FC rasmi wametangaza kuachana na mipango ya kumsajili aliyekuwa kiungo mchezeshaji fundi raia wa Kenya, Francis Kahata.

 

Awali, Azam na Yanga walitajwa kuingia kwenye vita ya kuwania saini ya kiungo huyo rasta ambaye hivi sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika wiki iliyopita kabla ya kurejea kwao Kenya.

 

Championi Ijumaa, limejiridhisha kwa mabosi wa Azam kuwa kiungo huyo hatasajiliwa huku wakiweka mipango mingine katika usajili wa msimu ujao.


Mmoja wa mabosi wa Azam alisema kuwa wana mikakati mizito ya kutengeneza kikosi imara kitakachofanya vizuri katika michuano ya kimataifa, mwakani.

 

Bosi huyo alisema kuwa tayari wana orodha ya wachezaji waliopo katika mipango yao lakini siyo Kahata ambaye hakuwa anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba.

 

“Kahata aliwahi kuletwa kwa uongozi kwa ajili ya kukamiliksha mipango ya kumsajili, lakini ikashindikana kutokana na mipango yetu tuliyokuwa nayo katika kukisuka kikosi kitakachokuwa imara na tishio.

 

“Hivyo Kahata rasmi tumesitisha mipango yetu ya kumsajili na badala yake tumemuacha aende kwingine, atakapotaka kwenda kucheza lakini siyo Azam,” alisema bosi huyo.


Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria alisema: “Muda wetu wa usajili bado na kila kitu kitajulikana mara baada ya ligi kumalizika.

SOMA NA HII  KUMBE ISHU YA DUBE IPO HIVI...KULIPA FAINI SH M810 ILI KUONDOKA AZAM...KAMATI YASHANGAZWA!!