Home Yanga SC YANGA YAHOFIA KUFANYA MAKOSA KWENYE USAJILI, HESABU ZAO HIZI HAPA

YANGA YAHOFIA KUFANYA MAKOSA KWENYE USAJILI, HESABU ZAO HIZI HAPA


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba makosa ambayo walifanya kwenye masuala ya usajili nyakati za nyuma hayatajirudia kwa kuwa wamejipanga kufanya mambo kwa utofauti.


Miongoni mwa wachezaji ambao walisajiliwa Yanga hivi karibuni ni pamoja na Wazir Junior ambaye amefunga bao moja na hana nafasi kikosi cha kwanza yupo Juma Balinya, Patrick Sibomana na Yikpe Gnamien ambao hawakuweza kufanya vizuri na walisepa kikosini mazima.

Wapo wengine ambao waliachwa licha ya kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na David Molinga ambaye alikuwa ni mshambuliaji aliyeletwa na Mwinyi Zahera aliyekuwa kocha wa wakati huo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa wameanza kuwatazama aina ya wachezaji ambao wanawahitaji ili kuwasajili ila hawatafanya makosa kama zamani.

β€œTumefanya makosa nyakati za nyuma hivyo kwa wakati huu hali hiyo haitajirudia kwa sababu tumempa jukumu la kufanya hivyo kocha, (Nassredine Nabi) wale wachezaji ambao atakuwa anahitaji basi tutawasajili.

β€œHao ina maana kwamba moja kwa moja wataingia kwenye kikosi cha kwanza. Kwa wale ambao sisi tutawaona tutamwambia mwalimu na kutazama ripoti yake kisha tutazungumza,” amesema Bumbuli.

Kuelekea kwenye usajili wa msimu ujao taarifa zinaeleza kuwa tayari Yanga imekamilisha usajili wa nyota wa AS Vita, beki Djuma Shaban ambaye atajiunga na timu hiyo Julai.

 

SOMA NA HII  MCONGO MWINGINE ANAYETAJWA KUTUA YANGA HUYU HAPA.....'DOGO' NI BALAA TUPU AISEE...