Home Azam FC STRAIKA MPYA AZAM AWAZIDI MASTAA WOTE WA SIMBA NA YANGA KWA MSHAHARA…

STRAIKA MPYA AZAM AWAZIDI MASTAA WOTE WA SIMBA NA YANGA KWA MSHAHARA…

Habari za Michezo

STRAIKA Mcolombia Franklin Navarro (24) aliyejiunga na Azam FC katika dirisha hili dogo la usajili akitokea Cortulua FC ya Daraja la Pili nchini kwao, atakuwa mchezaji wa pili wa Ligi Kuu Bara atakayekuwa akilipwa kibosi nyuma ya kipa Ali Ahamada ambaye naye ni mchezaji wa matajiri hao wa Chamazi.

Awali iliripotiwa  juu ya Ahamada kuwa mchezaji anayevuna mkwanja mrefu zaidi Ligi Kuu akikusanya zaidi ya Sh50 milioni mkwanja mrefu kuliko aliokuwa anapokea Bernard Morrison kutoka Yanga (sasa yupo FAR Rabat) na Stephane Aziz Ki waliokuwa wakikusanya takriban Sh23 milioni kwa mwezi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani inaelezwa straika huyo atakuwa akilipwa Dola 9,905 (ikiwa ni zaidi ya Sh24 milioni) huku akiahidiwa marupurupu mengine kibao ikiwa atafanya makubwa.

“Haikuwa kazi rahisi kuletwa nchini. Mabosi wameamua kuleta wachezaji wenye thamani kubwa kwa ajili ya kufanya mapinduzi kwenye soka la Tanzania na Afrika. Ukitaka kufanya vizuri hili haliepukiki,” kilisema chanzo ndani ya klabu hiyo kilichodokeza mchezaji huyo amesajiliwa kwa Dola 80,000 (zaidi ya Sh200 milioni).

Msimu huu, Navarro akiwa kwao Colombia amefunga bao moja na kutoa asisti mbili katika mechi 14. Kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo kunaonyesha dhamira ya Azam FC kuimarisha safu yake ya ushambuliaji na kuongeza utofauti kwenye kikosi chake chenye vipaji vya kimataifa.

Mashabiki na wapenzi wa Azam FC watakuwa na shauku ya kuona jinsi Navarro anavyoendana na aina ya uchezaji wa timu hiyo na kuchangia utendaji wao wa jumla katika mechi zijazo. Uwezo wake wa kupachika mabao na uchezaji wake unaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho, Azam FC inalenga kupata mafanikio katika mashindano ya ndani na nje ya nchi na ndio maana mabosi wa timu hiyo wapo makini kukusanya wachezaji wa daraja la juu huku wakimwaga mkwanja wa kutosha katika usajili.

SOMA NA HII  HABIB KYOMBO ARITHISHWA 'MIZIGO' YA MORRISON SIMBA...AANZA NAYO KAZI RASMI KWENYE MECHI NA WAARABU...