Home Yanga SC ISHU YA PLUIJM KURUDI YANGA IPO HIVI

ISHU YA PLUIJM KURUDI YANGA IPO HIVI

 


 HANS De Pluijm, kocha wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa hajafanya mazungumzo na kiongozi wa timu hiyo kwa sasa juu ya urejea kuinoa timu hiyo.

Hans De Pluijm ni moja kati ya makocha walioipa mafanikio Yanga chini ya utawala wake ambapo kwa sasa tayari timu hiyo imefuta benchi lake lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Cedric Kaze raia wa Burundi.

Habari zimekuwa zikieleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanafikiriwa kurejea ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Pluijm mwenye kadi ya uanachama wa Yanga.

Pia aliweza kufanya kazi na Singida United kwa mafanikio ya kuipeleka hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho na aliibuka ndani ya Azam FC ambapo huko hakudumu kwa muda.

Kocha huyo amesema:”Bado sijafanya mazungumzo na kiongozi yoyote kwa sasa kuhusu mimi kurejea ndani ya kikosi cha Yanga,” .




SOMA NA HII  SENZO :- SIMBA WANATAKIWA KUSHUKURU KUPATA SARE NA YANGA...LA SIVYO HALI INGEKUWA MBAYA KWAO...