Home Azam FC PRINCE DUBE NJE YA UWANJA WIKI MBILI

PRINCE DUBE NJE YA UWANJA WIKI MBILI


NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Prince Dube anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili ili aweze kurejea ndani ya uwanja.

 Dube mwenye mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC ambapo aliumia kwenye misuli ya paja dakika ya 25.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya bila kufungana baada ya dakika 90 kwa kuwa ubao ulisoma Mwadui 0-0 Azam FC baada ya dakika 90.

Kwa mujibu wa daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa amesema kuwa nyota huyo atakuwa nje kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurejea uwanjani.

“Dube atakuwa nje kwa muda wa wiki moja akipewa huduma na ile ya pili ataanza mazoezi mepesi ili kuweza kurejea kwenye ubora wake.

“Baada ya kukamilisha wiki hizo mbili akiwa nje ya uwanja atafanyiwa vipimo tena ili kujua kwamba kama yupo fiti kurejea kwenye mechi za ushindani ama atapaswa kusubiri tena, ila mashabiki wasiwe na hofu kila kitu kitakuwa sawa,” .

SOMA NA HII  DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI NA YANGA KUANZA....SOPU AJIAPIZA KUMFANYA MWANYETO ATELEZE TENA LEO...