Home Azam FC DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI NA YANGA KUANZA….SOPU AJIAPIZA KUMFANYA MWANYETO ATELEZE...

DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI NA YANGA KUANZA….SOPU AJIAPIZA KUMFANYA MWANYETO ATELEZE TENA LEO…


Mshambuliaji mwiba kwa mabeki wa Yanga, Abdul Seleman ‘Sopu’ amesema anatamani kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoivaa Yanga jumanne baada ya kutamba kuwa fiti kwa asilimia 100 huku akitamba ametumia mchezo dhidi ya Uganda kuimarisha mwili wake. 

Sopu aliye weka rekodi ya kumfunga mabao 3-0 kipa wa Yanga Djigui Diarra kwenye mchezo wa fainali kombe la shirikisho la Azam (FA) atakutana na mabimgwa hao watetezi kwenye mchezo wa ligi kuu Bara akiwa na Azam FC.

Sopu ambaye alikosekana kwenye michezo yote miwili ya Azam FC dhidi ya Kagera Sugara wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 na Geita Gold wakikubali sare ya bao 1-1 ameliambia mwanaspoti yupo tayari kuanza kazi dhidi ya Yanga jumanne.

“Nipo timamu kiafya na kimwili sasa hilo limethibitishwa kwenye mchezo wetu wa Uganda nikiwa na timu ya taifa pamoja na kukosa matokeo nilipata nafasi ya kucheza naamini kama nitapewa nafasi mechi ijayo naweza kuongeza nguvu kikosini”. Alisema na kuongeza ; “Utakuwa mchezo mzuri na waushindani na endapo nitapa nafasi ya kucheza. Natarajia kupewa ulinzi wa kutosha kutokana na kile nilicho kifanya nilipo kutana na Yanga  kwenye mechi ya mwisho wa fainali nikiwa na Coastal Union”.

Sopu alisema anawaheshimu Yanga na wanatarajia kupata mechi ngumu na yaushindani kutoka kwao huku akikiri dakika 90 za mchezo zita amua nan

SOMA NA HII  KUHUSU UVUMI WA KUMKATAA FEI TOTO...NABI AIBUKA NA KUANIKA KILA KITU WAZI...