Home Habari za michezo BAADA YA KUONA KIWANGO CHA MAYELE…MUSONDA KAKUNA KICHWA WEE…KISHA AKASEMA HILI..

BAADA YA KUONA KIWANGO CHA MAYELE…MUSONDA KAKUNA KICHWA WEE…KISHA AKASEMA HILI..

Habari za Yanga

Mshambuliaji mpya wa Wananchi, Kennedy Musonda amesema kuwa anaifahamu Yanga tangu miaka sita iliyopita wakati akicheza Zanaco FC ya nyumbani kwao Zambia.

Musonda amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV ikiwa ni mahojiano yake ya kwanza tangu ametua Tanzania kuwatumikia Mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania.

“Ninaifahamu Yanga tangu mwaka 2017, nilikuja hapa Tanzania na Timu yangu ya Zanaco kucheza michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika, nilishangaa kuona timu ina mashabiki wengi namna ile, sisi ni timu kubwa na ina mashabiki wengi.

“Wapo wachezaji baadhi wa Yanga ninaowafahamu kama kaka yangu Lazarous Kambole, yupo Aziz Ki ninamkubali sana, nilianza kumuona mwaka jana kwenye mashindano ya CAF, nilipenda magoli yake anavyofunga, mwingine ni Fiston Mayele, yule mtu ni hatari sana,” amesema Musonda.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- NI FEDHEHA KWETU KUWANGALIA YANGA WAKICHEZA...SIMBA TUNAPASWA KUAMKA..