Home Habari za michezo SAKATA LA KISINDA…YANGA NA TFF NI JINO KWA JINO…MABOSI JANGWANI WAIVIZIA TAARIFA...

SAKATA LA KISINDA…YANGA NA TFF NI JINO KWA JINO…MABOSI JANGWANI WAIVIZIA TAARIFA YA KAMATI KUAMSHA MOTO…


Inaelezwa kuwa Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umepanga kupeleka malamiko kwenye kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kugomea uamuzi wa TFF wa kuzuia Usajili wa Kisinda, huku wakiona kuna hujuma zinasukwa kupunguza makali ya timu yao.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Simon Patrick amesema; “Tulimsajili Tuisila Kusinda ndani ya muda, shirikisho la soka Tanzania (TFF) likatusaidia kupata (ITC) ndani ya muda.

“Tuliandika barua kuomba kufanyike replacement ndani ya muda kwa mujibu wa kanuni, kwa sababu madaktari wetu walituambia Lazarus Kambole bado hayuko fiti.

“Tunavyojua kamati bado haijakaa. Tumehuzunishwa sana na maamuzi ambayo TFF wamefanya kwenye usajili wa Tuisila Kisinda lakini sisi kama uongozi wa Yanga tumetuma maombi kwenye kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji na sio TFF.

“Tunasubiri taarifa rasmi ya KAMATI YA SHERIA NA HADHI YA WACHEZAJI ambayo ndio inajukumu la kushughulikia suala hilo,” amesema Patrick.

Swali la Mkule, Mtangazaji Wasafi FM “Ikitokea kamati ikatupilia mbali ombi lenu mtachukua hatua gani?

Jibu la Simon Patrick CEO wa Yanga SC. “Hapana hatuwezi kusema tutafanya nini kwa sababu bado hatujajibiwa…”

SOMA NA HII  DJUMA APEWA CHEO KIPYA YANGA..NTIBAZONKIZA, MAYELE WAWEKWA KANDO RASMI...