Home Uncategorized KUMBE ILE SARE YA MABAO 3-3 YA YANGA NA SIMBA, SIMBA WALILIA...

KUMBE ILE SARE YA MABAO 3-3 YA YANGA NA SIMBA, SIMBA WALILIA DAKIKA 15


BEKI wa Polisi Tanzania, Luccian William, ‘Gallas’ ambaye aliwahi kukipiga ndani ya Klabu ya Simba amefichua kuwa kwenye mechi waliyopindua mabao 3-3 mbele ya Yanga wachezaji walitumia dakika 15 kulia.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Oktoba 20,2013 Uwanja wa Taifa, Simba ilikwenda vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa imechapwa mabao matatu kwa bila.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas amesema kuwa wachezaji walikata tamaa na hakuna aliyekuwa na furaha kwa wakati huo zaidi ya kila mmoja kulia na Mungu wake ampe njia ya kutokea kwani mambo yalikuwa magumu.

“Hakuna aliyekuwa anaelewa nini kinaendelea kila mmoja alikuwa analia na Mungu wake ili ampe njia ya ya kutokea zile dakika 15 za mapumziko ilikuwa ni balaa.

“Ninakumbuka Kocha Mkuu, Kibadeni alisema, Gallas na Ndemla mkafanye mazoezi muingie ndani, mengine sikumbuki ila mwisho wa siku tuliweza kupindua matokeo na kuweka usawa wa kuwa 3-3,” amesema.

SOMA NA HII  JERO TU UTAONA MECHI KALI YA LEO, MZUMBE VIJANA CUP, TEGETA