Home Uncategorized HUYU HAPA KIUNGO MPYA WA SIMBA KUTOKA CONGO..ANAKIPIGA AS VITA

HUYU HAPA KIUNGO MPYA WA SIMBA KUTOKA CONGO..ANAKIPIGA AS VITA

SIMBA wameanza harakati za kumnasa kiungo nyota wa AS Vita Club ya DR Congo, Mukoko Tonombe, gazeti la  Mwanaspoti limebaini.

Hata kocha wa Vita, Florent Ibenge amethibitisha kwamba anaijua ishu hiyo ya Simba lakini anajua kwamba ni mchezaji mwenye mkataba hivyo anausikiliza uongozi.

Habari zinasema kwamba Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amewaambia viongozi kwamba anahitaji silaha zisizopungua nne kuimarisha kikosi hicho lakini muhimu zaidi ni kiungo mwenye supu kwenye miguu na mwili mkubwa.

Taarifa zinasema kwamba tayari Simba imeanza mchakato wa haraka wa kumpata staa huyo kwavile wamehakikishiwa kwamba ushindani ni mkubwa na wakienda taratibu hawawezi kumalizana naye kwa wakati.

Habari zinasema kwamba Simba tayari wameshazungumza na wakala wa mchezaji huyo na wanaendelea na mchakato huo ambao ukishakaa sawa watatua kwa uongozi wake muda wowote kuanzia sasa ingawa kocha anaonekana kushtushwa na uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka.

Hata hivyo, hesabu hizo za Simba pia zipo nchini Ghana ambako pia wanatafuta mtu mwingine sahihi atakayekuja kucheza sambamba na mzawa Jonas Mkude.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI