Home Uncategorized KOCHA MANCHESTER CITY AWAPA SOMO MASHABIKI NA WACHEZAJI KUHUSU CORONA

KOCHA MANCHESTER CITY AWAPA SOMO MASHABIKI NA WACHEZAJI KUHUSU CORONA


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa ni lazima kwa wachezaji na mashabiki kufuata kanuni za afya ili kujilinda na Virusi vya Corona.
Dunia nzima kwa sasa inapambana na maambukizi ya janga la Corona jambo ambalo limefanya ligi nyingi duniani kusimamishwa zikisubiri hali kuwa shwari.
Guardiola mwenye miaka 49 timu yake ya City ni mabingwa watetezi amesema kuwa dunia kwa sasa inapitia kipindi kigumu na kuna vingi inavikosa ikiwa ni pamoja na masuala ya mpira.
Wakati ligi inasimaishwa, City ilikuwa nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 28 na ina pointi 57 kibindoni na kinara ni Liverpool mwenye pointi 82  imecheza mechi 29. 
“Ni muhimu kwa kila mmoja kufuata kanuni na utaratibu wa wataalamu kwani hali sio shwari na kila mmoja anapitia wakati mgumu, kuna vingi tunavikosa lakini ni lazima tupambane,” amesema.
SOMA NA HII  BIASHARA UNITED MDOGOMDOGO WANAKUJA, MGORE ANA JAMBO LAKE