Home Uncategorized JACKSON MAYANJA: MAMBO BADO HAYAJWA SHWARI KWA SASA

JACKSON MAYANJA: MAMBO BADO HAYAJWA SHWARI KWA SASA


JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC kwa sasa anakipiga anakinoa kikosi cha KFC cha Uganda amesema kuwa hali bado haijawa shwari kutokana na Virusi vya Corona.

Mayanja kwa mwezi Februari alitwaa tuzo ya Kocha Bora ambapo alisema kuwa ilitokana na juhudi za wachezaji wake baada ya kukiongoza kikosi hicho kutoka kwenye nafasi ya 16 hadi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uganda pia amefanikiwa kukifikisha Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho nchini Uganda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa kumekuwa na utofauti baada ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo mambo mengi yamebadilika jambo ambalo linawafanya wachukue tahadhari ili wawe salama.

“Mambo yamebadilika na kila mmoja kwa sasa anachukua tahadhari, bado hatujajua mambo yatakuwa shwari lini lakini tunaomba Mungu kila kitu kiwe sawa,” amesema.


SOMA NA HII  YANGA YAITANGAZIA VITA JUMLAJUMLA SIMBA, MACHI 8 TAIFA