Home Habari za michezo YANGA SASA FRESH

YANGA SASA FRESH

Habari za Yanga

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiondolea klabu ya Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kumlipa mchezaji Gael Bigirimana.

Bigiramana alikuwa mchezaji wa Yanga, alifungua kesi FIFA baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

“Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili,” imeeleza taaifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

TFF pia imeeleza kuwa imefungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA WAWA KUTEMWA AU AACHWE...PAWASA AIBUKA NA HILI..ATOA ONYO KALI...