Home Simba SC KUYEYUKA KWA DABI, HAJI MANARA AOMBA MSAMAHA

KUYEYUKA KWA DABI, HAJI MANARA AOMBA MSAMAHA


Anaandika Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba:-

 Samahani!!


Ni neno moja lenye maana sana kwa muungwana.

Kuanzia Jumatatu hii nilizunguka kwenye vituo vya redio,televisheni na magazeti kufanya promotion kubwa kuelekea mchezo wa jana ambao ulikuja kuhairishwa baadae.

Sijilaumu kwa kile nilichofanya kwa niaba ya klabu yangu, lakini nimeumizwa sana kuona mashabiki wake hawakupata walichokitarajia.

Najihisi ni mkosaji na nadhani kuna haja ya kuwajibika kwa kitendo kile, nilitumia nguvu kubwa kuhakikisha tunajaza uwanja, lakini matokeo yake ni maumivu yaliyoacha doa kuu.

Nawaza kwa hisia, kwa nini sauti yangu iwe sehemu ya kuwapa maumivu wengine? Wangapi wamejeruhiwa kimwili nĂ¡ kiaikili kwa kilichotokea jana?

Naogopa na naomba msamaha sana kwa mashabiki wote hususani mliokuja jana kwa Mkapa. Binafsi nipo katika kipindi kigumu mno. Kila nikiwafikiria mashabiki wale ambao always, ndio huufanya mchezo huu wa soka kuwa hivi ulivyo sasa.

Inawezekana nisiwe nahusika hata kidogo kuhairishwa kwa mchezo ule, but, (lakini) nitakuwa mpuuzi nisiposema samahani kwenu, imani yangu taarifa rasmi ya klabu juu ya kadhia hii nzito itatolewa.

Mungu awabariki sana ndugu zangu.

SOMA NA HII  FT: SIMBA 2-0 ST GEORGE....KIBU NA OKWA WAFUNGA STAILI MOJA....CHAMA AMERUDIII..HUYO MZUNGU LABDA 'WAMLOGE'...