Home Uncategorized TSHISHIMBI:NASUBIRI SIMU YA MABOSI NISAINI

TSHISHIMBI:NASUBIRI SIMU YA MABOSI NISAINI

PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa kwa sasa anasubiri simu ya mabosi wa Yanga ili amalizane nao kwenye suala la kumwaga wino.

Tshishimbi mkataba wake ndani ya Yanga umebakisha miezi minne na kumekuwa na msuguano wa muda juu ya kusaini kwake ndani ya Yanga kwa kile ambacho amesema kuwa anatazama dau litakalokuwa mezani.

Nyota huyo amesema:”Nimeongea na mabosi wa Yanga na walitaka kunipa mkataba wa miaka miwili sikusaini kutokana na mambo kutokwenda sawa lakini waliniahidi kuwa watanipigia simu hivyo kwa sasa ninasubiri simu yao  ili nimalizane nao,” .

Habari zinaeleza kuwa tayari Tshishimbi ambaye ambaye inaelezwa kuwa Simba walikuwa mezani kuisaka saini yake ameshamalizana na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili.

SOMA NA HII  HILI NDILO BALAA LA NICOLAS WADADA WA AZAM FC