Home Geita Gold FC BAADA YA KUULILIA SANA ‘WEMBE’…NDOA YA GEITA GOLD NA MPOLE YAVUNJIKA RASMI…

BAADA YA KUULILIA SANA ‘WEMBE’…NDOA YA GEITA GOLD NA MPOLE YAVUNJIKA RASMI…

Klabu ya Geita Gold yenye maskani yake Mkoani Geita, imeachana na mshambuliaji wake George Mpole.

Geita Gold haikuweka wazi sababu hasa za kuvunja Mkataba na mpachika nyavu huyo aliechukua kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2021/2022 akimpiku Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele.

George Mpole alikuwa na mvutano na mabosi wa Geita Gold kwa miezi kadhaa huku akijitenga na timu kwa kile alichodai kuwa ni mgonjwa lakini pia anadai maslahi yake.

Mara kadhaa uongozi wa Geita Gold ulikanusha hadharani madai ya mchezaji huyo na hatimaye sasa ndoa ya wawili hao imefika tamati.

Kwa sasa Mpole yuko huru kujiunga na klabu yoyote.

SOMA NA HII  YANGA:- MMILIKI WA IHEFU KAUZIWA MZIGO WA BANGI.....