Home Habari za michezo YANGA:- MMILIKI WA IHEFU KAUZIWA MZIGO WA BANGI…..

YANGA:- MMILIKI WA IHEFU KAUZIWA MZIGO WA BANGI…..

Habari za Michezo leo

Ofisa Habari wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wamemaliza deni lao na timu ya Ihefu FC baada ya kuichabanga bao 5-0 katika Dimba la Azam Complex, jana Jumatatu, Machi 11, 2024.

Itakumbukwa kuwa, Ihefu ndiyo timu iliyofungwa na Yanga bao 2-1 msimu uliopita na kuiharibu unbeaten yao ya 49 kuelekea 50. Isitoshe, msimu huu, Ihefu ndiyo timu pekee ambayo imeifunga Yanga kwenye michezo yake yote 18 ambayo imecheza, hivyo Wananchi walikuwa na kila sababu ya kulipa kisasi hicho.

“Tumesikia Ihefu wana mmiliki mpya, huyu ni kama ameuziwa mzigo wa bangi bila kujua au amejenga kwenye makaburi ama mtu kanunua nyumba yenye mgogoro.

“Ihefu tulikuwa tunamtafuta kwenye 18 zetu, leo tumemalizana nao vizuri, tumempa kitu ambacho anatakiwa tuheshimiane huko mbeleni, hizi ni salam za kuheshimiana.

“Nilikuwa naongea na kocha Mexime nikamwambia wewe ni kocha mzuri na hizi bao ulizokula sio wewe tu, wapo wengine saba wewe ni wa nane ambao wamekula chumba tano. Kwa hiyo hata ukipita mtaani usijisikie vibaya, kuwa na amani kabisa, asijisikie unyonge,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA PILI NA BAMAKO...YANGA WAPANGA UMAFIA HUU KUMALIZA SHOW MAPEMA...