Home Habari za michezo BAADA YA DROW YA CAF…MAKOCHA SIMBA, YANGA WATIA NENO KUHUSU WAPINZANI WAO….

BAADA YA DROW YA CAF…MAKOCHA SIMBA, YANGA WATIA NENO KUHUSU WAPINZANI WAO….

Habari za Michezo leo

MAKOCHA wa klabu za Tanzania Simba na Yanga wamefunguka mara baada ya kumfahamu mpinzani wao katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika droo ya CAF iliyofanyika leo mchana huku Simba wanakutana kwa mara nyingine Al Ahly ya Misri na Yanga kucheza na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Baada ya droo hiyo Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema katika hatua hiyo hakuna kukwepa yoyote lazima watakutana naye na wanaenda kucheza kwa mara nyingine na Al Ahly.

Amesema hakuna mchezaji, benchi la ufundi hata viongozi wa Simba ambaye amfahamu Al Ahly tumeshakutana naye mara kadhaa na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.

“Tukumbuke hivi karibuni tulikutana naye katika Afrika Football League (AFL) kati ya timu nane tunaenda kutolewa kwao na bahati haikuwa kwetu. Sasa ni wakati wa kuchanga karata zetu vizuri kwenda kupambana naye.

Hatuna presha juu ya mechi ya nyumbani kikubea tunafanya maandalizi kwa ajili ya kuhakikisha tunafanikiw kusonga mbele kwa kujiweka imara kupambana na Al Ahly ambaye tunamfahamu vizuri akiwa ugenini na nyumbani,” amesema Matola.

Naye Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema wanakutana na timu bora Afrika na anaifahamu kwa sababu aliwahi kukaa Afrika kusini na kuhakikisha anapita katika misingi ya mpinzani wake kupata matokeo.

“Katika hatua hii hakuna mdogo wala mnyonge hakuna aliyefika kwa bahati bali alipambana na kufika hapa , tunamfahamu Mamelodi Sundowns sio timu ndogo tuko tayari kwa mchezo wa hatua ya robo,” amesema Kocha huyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDA JUZI...SASA MANDONGA NA MWAKINYO 'KULA SAHANI MOJA' ...ISHU IKO HIVI...