Home Azam FC DEAL DONE….MKANDARA AKAMILISHA SAFARI YAKE YA KUTUA AZAM FC….SASA MAMBO NI ‘BULIBULI’….

DEAL DONE….MKANDARA AKAMILISHA SAFARI YAKE YA KUTUA AZAM FC….SASA MAMBO NI ‘BULIBULI’….


Azam FC (@azamfc) imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala (@c.mkandala) kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Dodoma Jiji.

Kiungo huyo aliyefanya vizuri msimu uliopita, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa (@Yusufbakhresa) na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ (@abdulkarim.amin).

Mkandala, 21, ni mmoja wachezaji vijana wanaochipukia vizuri, amesaini mkataba huo wenye kipengele cha kuongeza ndani ya miezi sita na hiyo itatokana na kiwango atakachokionesha.

Aidha mbali na kuicheza Dodoma Jiji, Mkandala pia amewahi kucheza kwa misimu mitatu ndani ya kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons, 2018-2019 hadi 2020-2021.

Huo unakuwa usajili wa kwanza Azam FC kwa wachezaji wa ndani kuelekea msimu ujao.

Kabla ya Mkandala, tayari timu hiyo imeshawatangaza wachezaji watatu wa kigeni, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho, wanaotokea Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.

SOMA NA HII  BAADA YA KICHAPO CHA ZANACO...YANGA WAJIPOOZA LEO..WAICHAPA TIMU YA DARAJA LA KWANZA GOLI ZA KUTOSHA